Receive up-to-the-minute news updates on the hottest topics with NewsHub. Install now.

Makubwa jamani! Kutana na msichana wa miaka 5 anayetoka hedhi

October 11, 2017 6:03 AM
49 0
Makubwa jamani! Kutana na msichana wa miaka 5 anayetoka hedhi

Msichana wa miaka mitano New South Wales, nchini Australia ana maradhi yasiyokuwa ya kawaida ambayo yameufanya mwili wake kukua kwa hali isiyokuwa ya kawaida.

Emily Dover ana mardhi aina ya ‘Addison’s’, ambayo hubadilidha na kutatiza homoni za ukuaji wa mwili wa mtu.

Msichana huyo alianza kumea matiti akiwa na umri wa miaka miwili na kuanza kushuhudia hedhi akiwa na miaka minne. Pia, mwili wake una uzani wa kilo 44 na hukejeliwa shuleni kwa sababu ya unene wake.

Ili kuponya maradhi yake, madaktari wamempendekezea sindano za kila mwezi ili kuufanya mwili wake kuwa sawa na mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 50.

Wakati wakihojiwa, wazazi wa Emily walisema walikuwa wamegundua hali isiyokuwa ya kawaida ya mwanao wakati akiwa mchanga. Mama yake Tam alisem: "Hata ajapata nafasi ya kuwa msichana mdogo."

Alisema, walifanya kila waliloweza ili kuhakikisha Emily alipata maisha ya kawaida ya mtoto mchanga. Wameanzisha mchango wa fedha mtandaoni ili kusaidia kuchangisha fedha za matibabu yake.

Source: kiswahili.tuko.co.ke

Share in social networks:

Comments - 0